IS YAANGUSHA NDEGE YA KIJESHI SYRIA

IS YAANGUSHA NDEGE YA KIJESHI SYRIA

Like
448
0
Wednesday, 24 December 2014
Global News

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu Islamic State-IS, limeiangusha ndege ya kivita katika anga ya Syria ambayo, kwa mujibu wa shirika la kuchunguza Haki za Binadamu nchini humo, ni ya Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.

Shirika hilo lenye makao nchini Uingereza limesema IS imeidungua ndege hiyo karibu na mji wa Raqqa ulipo Kaskazini Mashariki mwa Syria, kwa kutumia kombora la kudungulia ndege.

Taarifa zaidi kutoka shirika hilo zimeeleza kuwa rubani wa ndege hiyo amekamatwa.

 

 

Comments are closed.