IS YASHUKIWA KUHUSIKA NA MAUAJI ANKARA

IS YASHUKIWA KUHUSIKA NA MAUAJI ANKARA

Like
218
0
Tuesday, 13 October 2015
Global News

WAZIRI mkuu wa Uturuki Ahmet Davotuglo amesema kuwa wachunguzi wa nchi hiyo wanakaribia kumtambua mmoja kati ya washambuliaji wa kujitoa muhanga wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya maandamano ya amani katika kituo cha treni yaliyowaua watu wasiopungua 97 mjini Ankara.

Davutoglu amesema kwamba kundi la dola la Kiislamu limepewa kipaumbele katika uchunguzi huo kwa kushukiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa.

Wakati hayo yakijiri katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameihimiza Uturuki iwe makini katika njia inazozitumia kuyashughulikia mashambulizi ya kigaidi.

          

Comments are closed.