IVORY COAST: KESI DHIDI YA MKE WA GBAGBO YAANZA

IVORY COAST: KESI DHIDI YA MKE WA GBAGBO YAANZA

Like
298
0
Tuesday, 31 May 2016
Local News

Kesi ya mashtaka ya ukiukaji wa kibinaadamu dhidi Mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Simone Gbagbo,imeanza katika mahakama ya mji mkuu wa Abidjan.

Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama ‘mwanamke mkakamavu’ amewahi kuhudumia miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3.

Vita hivyo viliisha baada ya mumewe, Laurent Gbagbo kukamatwa na Umoja wa Mataifa na jeshi la ufaransa kumuunga mkono rais wa hivi sasa Rais Alassane Ouattara.

Bwana Gbagbo anakabiliwa na mashtaka ya kivita na mahakama ya kimataifa ya ICC wawili hao wamekana madai hayo.

Comments are closed.