Ivory Coast imefunga ukurasa wa kombe la mataifa ya Afika AFCON kwa kuibuka na ushindi dhidi ya majirani wake wa Ghana kwa mikwaju ya penati ya 9-8 kwenye ardhi ya Equatorial Guinea ndani ya jiji la la Bata baada ya kutoka sare ya bila kufungana
“tunaupeleka huu ushindi kwa waivory coast” alisema kocha mfaransa Herve Renard ambae pia aliipatia ushindi Zambia dhidi ya Ivory Coast katika fainali za mwaka 2012
Ushindi huo wa Ivory Coast na Zambia chini ya Herve Renard unamfanya kocha huyo aingie kwenye rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa kombe la mataifa ya Afrika akiwa na mataifa tofauti
Ushindi huo wa jana ni wa pili kwa timu ya Ivory Coast ambapo kwa mara ya kwanza walitwaa taji hilo mwaka 1992 ambao pia waliupata dhidi ya Ghana kwa njia ya penati baada ya kutoka sare ya magoli
Mashabiki wa mchezo wa soka nchini Ivory Coast wamekuwa wakisubiri ushindi huo kwa takribani miaka 23 bila kukata tama badala yake waliiunga mkono na kuipa hamasa timu yao hadi hii leo wamerejesha ushindi nyumbani