JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

Like
326
0
Tuesday, 07 October 2014
Slider

SHIRIKISHO la kandanda Tanzania Tff,limesema mashindano ya taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12, yatafanyika mkoani mwanza kuanzia mwezi Desemba mwaka huu,ukiwa ni mpango maalumu unaolenga kupata kikosi imara cha kitakachoshiriki michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya 17 (U17), mwaka 2019, ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Akizungumza na wanahabari hii leo kuelezea mpango huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi,amesema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote Tanzania,lakini kwanza amenza kwa kusema yeye pamoja na kamati yake ya utendaji ipo madarakani kuendeleza soka na si kulumbana .

Kwa upande wao mkurugenzi wa shule za Alliance,James Bwire, pamoja na Kanali mstaafu Idd Kipingu wa Lord Baden,wameridhia kwa kauli moja vituo vyao kutumika katika kuendeleza soka la Tanzania,na kipingu akisisitiza kuwa suala hili ni la watanzania wote.

Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350.

Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo

Comments are closed.