JAMII IMEOMBWA KUTAMBUA UWEPO WA WATOTO YATIMA NA WALIOTELEKEZWA

JAMII IMEOMBWA KUTAMBUA UWEPO WA WATOTO YATIMA NA WALIOTELEKEZWA

Like
238
0
Thursday, 20 August 2015
Local News

UONGOZI wa Kituo cha kulelea watoto wadogo wakiwemo yatima na waliotelekezwa na wazazi, Msimbazi centre wameiomba serikali, jamii na Taasisi mbalimbali kutambua uwepo wa watoto hao.

 

Akizungumza na EFM jijini Dar es Salaam mlezi wa kituo hicho sista Anna Francis amesema miongoni mwa watoto waliopo hapo ni wale waliotupwa na mama zao pindi wanapojifungua kwa visingizio mbali mbali.

 

Aidha sista Anna amesema kuwa mbali na kutopata misaada kutoka sehemu mbalimbali kwa sasa kituo hicho kina watoto arobaini na moja wanaopatiwa huduma.

 

Comments are closed.