JAMII IMEOMBWA KUTOWADHARAU NA KUWANYANYAPAA WAGONJWA WA SIKO SELI

JAMII IMEOMBWA KUTOWADHARAU NA KUWANYANYAPAA WAGONJWA WA SIKO SELI

Like
303
0
Wednesday, 19 August 2015
Local News

JAMII imeombwa kutowadharau na kutowanyanyapaa Wagonjwa wa Siko Seli na badala yake kuwasaidia kutibu hali zao kwa kuwa asilimia 13 ya Watu wote Nchini wana vinasaba vya ugonjwa huo ambapo Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 5 duniani kuwa na Wagonjwa wengi zaidi.

 

Wito huo umetolewa leo katika Uzinduzi wa Mpango wa Miaka 3 wa kupima Watoto wachanga Siko Seli utakaoenda Sanjari na Bonanza la Michezo kuadhimisha Mwezi wa kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo uliondaliwa na Taasisi binafsi ya Siko Seli Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Wadau wengine.

 

Balozi wa Siko Seli Tanzania Honeymoon Aljabir amesema lengo la zoezi hilo ni kuokoa maisha ya Watoto wa chini ya miaka 5.

 

Comments are closed.