JAMII IMEOMBWA KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA HATARISHI

JAMII IMEOMBWA KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA HATARISHI

Like
260
0
Wednesday, 02 March 2016
Local News

JAMII nchini imeombwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kupunguza vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto hao.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Afisa Ustawi wa jamii Neema Mambosho wakati alipokuwa akizungumza na E FM juu ya ongezeko la watoto wa mtaani.

Amesema kuwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za ukatili na kunyanyapaliwa hivyo jamii inapaswa kuelimishwa ili kuzuia vitendo hivyo.

Comments are closed.