JAMII IMETAKIWA KUEPUKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

JAMII IMETAKIWA KUEPUKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Like
269
0
Wednesday, 23 March 2016
Local News

KATIKA kupambana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi ikiwemo ongezeko kubwa la Joto Duniani, Mamlaka ya hali ya hewa kwa kushirikiana na Wakala wa misitu Nchini, wameitaka jamii kuepuka uharibifu wa mazingira na kuongeza kasi ya upandaji miti .

 

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Nchini Dokta Agness Kijazi alipozungumza na Waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya hali ya hewa Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 23mwezi wa tatu Duniani kote ambapo kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema ‘Joto kali, ukame, mafuriko kabiliana na mabadiliko yajayo’.

Comments are closed.