JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINAZOTOA HUDUMA KWA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZINAZOTOA HUDUMA KWA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Like
272
0
Thursday, 13 August 2015
Local News

JAMII imetakiwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa watoto yatima na wanao ishi katika  mazingira magumu kwani kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza ongezeko la idadi kubwa ya watoto wa mitaani.

 

Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa kituo kinacholea watoto wanaoishi katika mazingira magumu –BABA WATOTO CENTER–  MGUNGA MNYENYELWA amesema kuwa mpaka sasa wameweza kulea watoto 200  kituoni hapo pamoja na kuwapatia  mafunzo mbalimbali yanayohusu stadi za maisha.

 

Amebainisha kuwa Miongoni mwa mafunzo wanayopewa  kituo ni kutoa nafasi kwa watoto wa kike kujifunza ufundi cherehani ingawa harakati hizo zimekumbana na changamoto ya upungufu wa fedha za kununulia vifaa vya mafunzo.

Comments are closed.