JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKISHA WANAWAKE KIKAMILIFU KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI

JAMII IMETAKIWA KUSHIRIKISHA WANAWAKE KIKAMILIFU KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI

Like
332
0
Tuesday, 12 April 2016
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amewataka watanzania wote kutambua kwamba mafanikio na maendeleo yoyote ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla hayawezi kupatikana endapo wanawake hawataweza kushirikishwa kikamilifu kwenye vikao vya maauzi.

 

Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wanawake katika uongozi lililoandaliwa na taasisi ya uongozi na kuwakutanisha wanawake wa kitanzania wenye nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini.

 

Katika mkutano huo pia ameeleza kuwa ni jukumu la kila kiongozi kwa nafasi aliyonayo kuhakikisha anatumia nafasi hiyo kuwahamasisha na kuwawezesha wanawake wa Tanzania kwa kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kujikomboa kiuchumi.

Comments are closed.