JAMII IMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO

JAMII IMETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Like
318
0
Thursday, 03 March 2016
Local News

WAZAZI na Walezi nchini wametakiwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na ndugu au wanafamilia dhidi ya watoto wa kike na hata wa kiume ili wachukuliwe hatua.

Akizungumza na Efm Mwanasheria Msaidizi wa Jaji kutoka Chama cha Majaji Wanawake Tanzania-TAWJA-Koku Mwanemile ameeleza kuwa kufumbia macho vitendo hivyo kunachangia kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji kwa watoto.

Koku amebainisha kuwa endapo wazazi, walezi na jamii wataungana pamoja kwa kufichua vitendo hivyo vinavyosababisha athari kubwa kwa watoto itasaidia kupunguza vitendo hivyo na kuviondoa ndani ya jamii.

Comments are closed.