JAMII IMETAKIWA KUTOWANYANYAPAA WATU WENYE ALBINISM

JAMII IMETAKIWA KUTOWANYANYAPAA WATU WENYE ALBINISM

Like
234
0
Wednesday, 09 September 2015
Local News

WITO umetolewa kwa jamii kutowanyanyapaa Watu wenye albinism na badala yake kuwalinda na kuwathamini kama watu wa kawaida kabla ya baada ya uchaguzi kwa kuwa maisha yao yamekuwa hatarini mara kwa mara kutokana na fikra potofu na imani za kishirikina zinazosambazwa na baadhi ya watu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika hafla ya kukabidhi msaada wa carton 35 za mafuta ya kutunza ngozi na miwani 100 za jua zenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa ajili kuwasaidia waweze kujikinga na saratani mbalimbali zinazosababishwa na mwanga wa jua.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba amesema msaada huo umekuja kutokana na benki hiyo kuguswa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa kwa watu wenye albinism na kuamua kutoa msaaada huo katika maadhimisho yao yakutimiza miaka miwili.

Comments are closed.