JAMII IMETAKIWA KUUNGA MKONO UKUZAJI WA VIPAWA

JAMII IMETAKIWA KUUNGA MKONO UKUZAJI WA VIPAWA

Like
270
0
Friday, 26 February 2016
Local News

JAMII nchini imetakiwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanya na baadhi ya taasisi zinazo jihusisha na utoaji wa ujuzi na uendelezaji wa vipawa vya watoto na vijana ili kujenga jamii yenye tabia ya kujitegemea .

Hayo yamebainishwa na Mkude Kilosa ambaye ni  mkurugenzi msaidizi wa kituo cha kulelea watoto na vijana cha baba watoto kilichopo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na efm  juu ya maandalizi ya tamasha la wazi la sarakasi tamasha lililolenga kukuza na kuendeleza ujuzi wa vijana katika Nyanja zote  .

KILOSA amesema kuwa tamasha hilo litakalofanyika kesho jumamosi katika viwanja vya art space vilivyopo mikocheni litakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali za jijin Dar es salaam ili wawexe kubadilishana mawazo lakini pia kupata elimu ya namna ya kujikomboa kifikra.

Comments are closed.