JAMII YA WAFUGAJI PWANI YAOMBA KUTENGEWA MAENEO KUEPUSHA MOGOGORO

JAMII YA WAFUGAJI PWANI YAOMBA KUTENGEWA MAENEO KUEPUSHA MOGOGORO

Like
245
0
Tuesday, 24 March 2015
Local News

JAMII ya Wafugaji katika kijiji cha Mindukeni Kata ya Talawanda Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,wameomba kutengewa maeneo yao ili kuepusha migogoro inayojitokeza baina yao na Wakulima ikiwemo kujeruhiwa na Kuuwawa.

Ukosefu mpango wa matumizi bora ya ardhi, umesababisha kundi hilo la wafugaji kutengwa kushiriki kwenye shughuli za Kimaendeleo ndani ya  vijiji vyao.

Jamii hiyo ya Wafugaji wamefikisha kilio chao,mbele ya Mbunge wa jimbo hilo RIDHIWANI KIKWETE wakati akiwa kwenye ziara yake katika Kata ya Talawanda.

Comments are closed.