JAMII YATAKIWA KUFUATILIA KWA UMAKINI ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

JAMII YATAKIWA KUFUATILIA KWA UMAKINI ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Like
233
0
Thursday, 21 May 2015
Local News

JAMII imetakiwa kufuatilia kwa makini zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kushiriki ipasavyo kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo itagundua kasoro yoyote katika zoezi hilo ili hatua stahiki zichukuliwe. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akijibu swali la mbunge wa Mkanyageni mheshimiwa MOHAMED MNYAA juu ya uwepo wa uandikishaji wa watu wasiohusika kupiga kura hususani Zanzibar katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo. Waziri PINDA amesema kuwa endapo jamii itashiriki kikamilifu katika zoezi hilo itasaidia kwa kiasi kikubwa shughuli za uandikishaji kuwa za uhakika na zenye kuleta usawa kwa kila anayestahili kupiga kura na kuondoa kero zote kwa wahusika.

Comments are closed.