JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUDHIBITI MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUDHIBITI MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Like
213
0
Thursday, 05 March 2015
Local News

JAMII nchini imetakiwa kushirikiana na Serikali katika kudhibiti tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana kuanzia ngazi ya Familia kwakuwa  vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji wa kata ya Temeke Elias Wawa amesema kuwa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya linaanzia katika ngazi ya familia hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuzungumza na vijana wao ili kuondokana na tatizo hilo .

Aidha amewataka wazazi kutowakatisha tama vijana pale wanaposhindwa kutimiza maazimio yao na badala yake wawasaidie kimawazo na ikiwezekana kifedha kufanya shughuli mbadala ili kujiingizia kipato na kuweza kujimudu ili kuepuka kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

Comments are closed.