JAMII YATAKIWA KUZINGATIA USAFI KUEPUKA KIPINDUPINDU

JAMII YATAKIWA KUZINGATIA USAFI KUEPUKA KIPINDUPINDU

Like
204
0
Friday, 28 August 2015
Local News

JAMII imetakiwa kuzingatia usafi wa mwili, chakula na mazingira yanayowazunguka kwa kuwa hali ya usafi jijini Dar es salaam na mikoa jirani sio ya kuridhisha kufuatia mlipuko wa Kipindupindu kuendelea kusambaa kwa kasi ambapo hadi sasa idadi ya Wagonjwa waliopokelewa vituoni imefikia 385 huku Mkoa wa Pwani ukiripotiwa kuwa na wagonjwa saba na kifo cha Mtu mmoja.

Hayo yamesemwa leo jijjini Dar es salaam wakati wa makabidhiano ya msaada wa nyenzo za ziada za box 1,000 ya dawa za waterguard zenye thamani ya shilingi milioni 42 za kitanzania pamoja na misaada mingine ya kitaauluma baina ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Shirika la la Afya Duniani -WHO.

Comments are closed.