JANETH RITHE AJIUNGA NA ACT

JANETH RITHE AJIUNGA NA ACT

Like
343
0
Thursday, 23 July 2015
Local News

ALIEKUA Diwani wa Kata ya Kunduchi kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA- ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho -BAWACHA-jimbo la Kawe Janeth Rithe ameachana na chama hicho na  kujiunga na chama cha ACT  WAZALENDO  akiambatana na Viongozi wenzake 12 wa jimbo la Kawe.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama cha ACT WAZALENDO  Rithe amesema amechukua uamuzi huo  baada ya kusoma sera na kugundua kua hicho ndio chama kinachosimamia demokrasia ya kweli tofauti na vyama vingine vya siasa.

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa ACT WAZALENDO  Msafiri Mtemelwa amesema kila  Mtanzania ana haki ya kuhamia ama kujiunga na chama chochote anachokitaka kwani vyama hivyo sio dini.

Comments are closed.