JAPAN KUCHUNGUZA SAUTI INAYOHISIWA KUWA NI YA MWANDISHI ALIESHIKILIWA MATEKA NA IS

JAPAN KUCHUNGUZA SAUTI INAYOHISIWA KUWA NI YA MWANDISHI ALIESHIKILIWA MATEKA NA IS

Like
177
0
Thursday, 29 January 2015
Global News

JAPAN inachunguza sauti iliyorekodiwa ambayo inawezakana ni ya mwandishi wa habari wa Japan aliyeshikiliwa mateka na wapiganaji wa Islamic state.

Sauti hiyo inarudia tishio la kumuua rubani wa Jordan aliyetekwa mateka na wapiganaji hao hadi Jordan itakapomwachia huru mwanamke wa Iran aliyehusika na shambulizi la bomu.

Famili ya Rubani na mpiganaji mwenye asili ya Jordan anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa hao wameendelea kuweka shinikizo kwa Serikali ya Jordan kufanya kila iwezalo kuokoa maisha yake.

Jordan imeahidi kumuachia mwanamke huyo lakini Mjomba wa Rubani anasema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa wanamgambo wa IS kuwa hawataki kupokea ahadi hiyo na kuwa watamuua siku ya Alhamisi, leo.

 

Comments are closed.