JAPAN YAKUMBUKA SHAMBULIO LA HIROSHIMA

JAPAN YAKUMBUKA SHAMBULIO LA HIROSHIMA

Like
399
0
Thursday, 06 August 2015
Global News

RAIA wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima.

Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.

Katika hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia.

JAP2

 

Comments are closed.