JENGO LAANGUKA LAUA KUMI

JENGO LAANGUKA LAUA KUMI

Like
303
0
Tuesday, 25 November 2014
Global News

  

WATU KUMI wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza kuwa Watu saba wamejeruhiwa pia baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku.

Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi.

Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ni ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi.  Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo hilo wameondoka katika makazi yao kwa nia ya kujihadhari.

Comments are closed.