JESHI LA NIGERIA LABOMOA MADHABAHU YA KISHIA

JESHI LA NIGERIA LABOMOA MADHABAHU YA KISHIA

Like
205
0
Monday, 14 December 2015
Global News

KUNDI kuu la kiislamu nchini Nigeria linaloungwa mkono na waislamu wa Kishia wa Iran, linasema kuwa mke wa kiongozi mkuu Sheikh Ibrahim Zakzaky, ameuwawa katika makabiliano na jeshi kaskazini mwa mji wa Zaria.

 

Vuguvugu la kiislamu nchini Nigeria (IMN) linadai kuwa Zeenat Ibraheem ameuwawa kwa pamoja na mwanaye Sayyid Ibraheem Zakzaky.

 

Sheikh Zakzaky alikamatwa na wanajeshi waliozingira nyumba yao kufuatia madai kuwa wanachama wa kundi hilo walijaribu kumuua kamanda mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai huko Zaria siku ya Jumamosi.

Comments are closed.