JESHI LA NIGERIA LAMNASA KINGOZI WA KUNDI LA ANSARU

JESHI LA NIGERIA LAMNASA KINGOZI WA KUNDI LA ANSARU

Like
246
0
Monday, 04 April 2016
Global News

JESHI la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.

Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatia kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni kwa Khalid al Barnawi.

Comments are closed.