JESHI LA NIGERIA LAWAOKOA WATU 180

JESHI LA NIGERIA LAWAOKOA WATU 180

Like
166
0
Monday, 03 August 2015
Global News

JESHI la Nigeria linasema kuwa limewaokoa zaidi ya watu 180, wengi wao wanawake na watoto, kutoka kwa kundi hatari la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, katika jimbo la Borno.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji moja wa jeshi amesema kuwa kambi kadhaa za waasi hao zilizoko karibu na mji wa Maiduguri zimeharibiwa na kamanda mmoja wa Boko Haram kukamatwa, lakini duru hizo hazijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.

Wakati hio huo, Rais wa Niger, Mahmadou Issoufou, amesema kuwa jeshi jipya linalojumuisha wanajeshi kutoka mataifa kadhaa huko Afrika magharibi, lina uwezo mkubwa wa kukabiliana na Boko Haram.

 

 

Comments are closed.