JESHI LA POLISI DODOMA YATANGAZA KUTOA MILIONI 5 KWA ATAKAEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA

JESHI LA POLISI DODOMA YATANGAZA KUTOA MILIONI 5 KWA ATAKAEFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAUAJI KATIKA KITUO CHA MAFUTA

Like
327
0
Friday, 07 August 2015
Local News

JESHI la polisi mkoani Dodoma limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni tano kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi waliohusika na tukio la mauaji ya walinzi wawili katika kituo cha mafuta cha state oil kilichopo eneo la kisasa manispaa ya Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma DAVID MISIME amesema majambazi hao wamefanya uharifu huo na kufanikiwa kupora vitu mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 10

Aidha kamanda misime ameiasa jamii hasa wale wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu watambue kuwa uhalifu haulipi na mwisho wake ni kuishia kwenye mikono ya dola na hatimaye kufugwa.

Comments are closed.