JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 50 KWA RAIA MWEMA ATAKAYETOA TAARIFA YA UHAKIKA ITAKAYOPELEKEA KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA SITAKI SHARI

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 50 KWA RAIA MWEMA ATAKAYETOA TAARIFA YA UHAKIKA ITAKAYOPELEKEA KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA SITAKI SHARI

Like
404
0
Tuesday, 14 July 2015
Local News

JESHI la Polisi nchini limetangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni hamsini kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa ya uhakika itakayofanikisha kukamatwa kwa majambazi waliowaua askari na raia pamoja na kuiba  silaha katika kituo cha polisi cha sitaki shari kilichopo Ukonga jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamishna wa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema kuwa jeshi la polisi limeona ni muhimu kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwa kutoa zawadi hiyo kwa kuwa suala la ulinzi na usalama ni la wananchi wote.

KOVA amesema mtu yeyote atakayepata taarifa za uwepo  wa wahalifu hao atoe taarifa kwa kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, msemaji wa Jeshi hilo na Mkurugenzi wa makosa ya jinai.

M13

Comments are closed.