JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUKAMATA SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KATIKA KITUO CHA SITAKISHARI

JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUKAMATA SILAHA ZILIZOPORWA NA MAJAMBAZI KATIKA KITUO CHA SITAKISHARI

Like
582
0
Monday, 20 July 2015
Local News

JESHI la Polisi Nchini limefanikiwa kukamata silaha zilizoporwa na majambazi katika kituo cha Polisi Sitakishari pamoja na fedha kiasi cha shilingi milioni 170.

 

Katika Operesheni hiyo Jeshi lilifanikiwa kukamata watuhumiwa watano ambapo wawili walipoteza maisha katika mapambano pamoja na silaha 16,  14 zikiwa za Staki shari, risasi 53 ambazo kati yake 28 zinatoka katika kituo hicho cha polisi, Stakishari.

 

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu wa Dar es salaam Suleiman Kova, amesema silaha hizo zimepatikana baada ya kupata taarifa katika kijiji cha Mandi Mkongo Kata ya Bupu Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani katikati ya Msitu ambako kikosi cha polisi kilifukua ardhini na kukuta silaha 15.

kova

 

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu wa Dar es salaam Suleiman Kova

Comments are closed.