JESHI LA POLISI LIMEIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA VIFAA

JESHI LA POLISI LIMEIOMBA SERIKALI KUWAONGEZEA VIFAA

Like
254
0
Wednesday, 28 January 2015
Local News

JESHI la Polisi nchini limeiomba Serikali kuwaongezea vifaa ili kuongeza ufanisi katika kupambana na makundi yanayovuruga amani kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Rais, Wabunge na Madiwani.

 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ERNEST MANGU kwenye mkutano wa mwaka wa jeshi hilo uliofanyika mjini Dodoma, kwa kujumuisha maofisa wakuu wa Polisi ili kutathimini utendaji kazi kwa mwaka uliopita na kuangalia mahali walipokosea kwa ajili ya kurekebisha.

 

Amebainisha kuwa hivi sasa wahalifu wamekuwa wakitumia mbinu mpya kwa ajili ya kufanya uhalifu jambo ambalo jeshi limejipanga kukabiliana nalo.

 

Comments are closed.