JESHI LA POLISI LIMESHAURIWA KUZISOMA NA KUZIELEWA SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI

JESHI LA POLISI LIMESHAURIWA KUZISOMA NA KUZIELEWA SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI

Like
198
0
Thursday, 30 July 2015
Local News

JESHI la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza ili kuliepushia lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani.

 

Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini katika Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.

 

Amesema Jeshi hilo linawajibu wa kuhakikisha Sheria za nchi zinafuatwa lakini jambo la msingi ni kuzielewa kabla ya kuzitekeleza.

 

 

Comments are closed.