JESHI LA POLISI TEMEKE KUFANYA MKUTANO NA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WGENI

JESHI LA POLISI TEMEKE KUFANYA MKUTANO NA WAMILIKI WA NYUMBA ZA KULALA WGENI

Like
269
0
Friday, 07 November 2014
Local News

JESHI la polisi mkoa wa Kipolisi Temeke limesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano mkubwa na wamiliki wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika mkoa huo ili kuweka mikakati mbalimbali ya kuzuia mauaji ya wanawake yanayotokea  katika baadhi ya nyumba hizo.

 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Temeke Kehenya Kehenya wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

 

Amebainisha kuwa wanawake hao waliuwawa katika matukio tofauti na vifo vyao wote vimefanana kwani wameuwawa kwa kunyongwa shingo  hivyo amewataka wamiliki hao wachukue taarifa kumbukumbu sahihi za wateja wao.

Comments are closed.