JESHI LAPEWA JUKUMU LA KUTENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6

JESHI LAPEWA JUKUMU LA KUTENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6

Like
301
0
Tuesday, 12 April 2016
Local News

JESHI La Magereza nchini na Jeshi la Kujenga Taifa wamepewa jukumu la kutengeneza madawati yenye thamani ya shilingi Bilioni 6 ambayo yatasambazwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

 

Jukumu hilo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama limetolewa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi ya makabidhiziano ya mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 6 kutoka Sekretarieti ya Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania fedha ambazo zimepatikana kufuatia kubana matumizi ya uendeshaji wa Ofisi hiyo.

 

Rais Magufuli amesema kuwa Ofisi ya Bunge pamoja na Watendaji wake wameonesha moyo wa kizalendo kwa Taifa kwani wametekeleza kwa vitendo maelekezo ya kubana matumizi ya fedha za Serikali.

Comments are closed.