Jiji la Mbeya Kuwaka Moto, leo kati ya Mbeya City VS Prisons

Jiji la Mbeya Kuwaka Moto, leo kati ya Mbeya City VS Prisons

Like
710
0
Sunday, 13 May 2018
Local News

Ni vita kubwa leo jiji Mbeya, ambapo pale wafalme wawili  katika jiji hilo, Mbeya City na Tanzania Prisons.

Watakapokutana kwenye mchezo wa ligi kuu kutafuta point 3.

Mbeya City wanaingia katika mchezo huo wakiwa wameachwa alama 15 na Tanzania Prisons walio na 44 kwenye msimamo wa ligi.

 

Wakati huo Mbeya City wao wamejikusanyia jumla ya pointi 29 pekee katika michezo 27 waliyocheza msimu huu.

 

Taarifa kutoka jijini Mbeya zinaeleza wadau na mashabiki wengi wanausubiria kwa hamu mchezo huo wa vuta nikuvute.

 

Kueleka mechi hiyo, baadhi ya wadau wameipa Prisons nafasi kubwa ya kupata matokeo kutokana na ubora walionao dhidi ya wapinzani msimu huu.

 

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni na itarushwa mubashara na kituo cha Azam TV.

 

Mechi nyingine ni ile ya morogoro ambapo Mtibwa itakuwa inaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro leo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *