SERIKALI kwa kushirikiana na Wananchi wametakiwa kuendeleza jititihada zinazofanywa na wadau mbalimbali nchini,hasa katika kuhakikisha wanazuia na kupunguza vifo vya Akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Changamoto hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya Afya nchini-AMREF health Africa,mkoani Simiyu GODFREY MATUMU,wakati wa mkutano wa kufunga Mradi wa Uzazi Uzima.
Amesema kuwa mashirika au taasisi binafsi ambazo zimekuwa zikijihusisha na masuala ya Afya zimekuwa zikibeba mzigo mkubwa katika kuhakikisha vifo hivyo vinapungua ,huku Serikali na jamii wakibaki kuwa ni watazamaji wa juhudi hizo.