JK AMTEUA ANTHONY MAVUNDE KUWA MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA

JK AMTEUA ANTHONY MAVUNDE KUWA MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA

Like
240
0
Tuesday, 26 May 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE amemteua ANTHONY MAVUNDE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
          Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam imesema kuwa Rais amefanya uhamisho wa wakuu  wa Wilaya kumi kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.


            Katika mabadiliko hayo amemhamisha Luteni EDWARD OLE LENGA kutoka Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa Mkoani Kagera ambapo amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali BENEDICT KITENGA aliyefariki dunia Aprili 20 mwaka huu.

Comments are closed.