JK AMWAPISHA KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

JK AMWAPISHA KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Like
289
0
Wednesday, 27 May 2015
Local News

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,  amemwapisha Katibu Mkuu mpya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula.

 

Aidha, katika sherehe fupi ya uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwapisha Balozi Hassan Simba Yahya kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

 

Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, Rais Kikwete amemwapisha pia Ndugu Hemed Idd Mgaza kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia.

 

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Balozi Mulamula alikuwa Balozi wa Tanzania Washington, Marekani.

Comments are closed.