JK ATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KANDA YA AFRIKA WA UENDESHAJI WA SHUGURI ZA SERIKALI KWA UWAZI

JK ATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KANDA YA AFRIKA WA UENDESHAJI WA SHUGURI ZA SERIKALI KWA UWAZI

Like
195
0
Tuesday, 19 May 2015
Local News

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA KIKWETE anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi –OGP.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 

Aidha taarifa imeeleza kuwa dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

Comments are closed.