JK ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KIMATAIFA KUCHUNGUZA JINSI YA KUGHARIMIA ELIMU DUNIANI

JK ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KIMATAIFA KUCHUNGUZA JINSI YA KUGHARIMIA ELIMU DUNIANI

Like
227
0
Friday, 09 October 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Kimataifa ya Kuchunguza Jinsi ya Kugharimia Elimu Duniani.

Tume hiyo, inayoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Elimu Duniani ina jumla ya wajumbe 30, wakiwemo marais na mawaziri wakuu wa zamani, wataalum wa elimu, wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali duniani.

 

Tume hiyo italenga kuangalia jinsi gani dunia inavyoweza kuongeza uwekezaji katika elimu katika muda mfupi na katika muda mrefu na itapendekeza aina ya uwekezaji na hatua za kuchukuliwa.

Comments are closed.