JK ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA WA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

JK ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA WA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

Like
512
0
Friday, 22 January 2016
Local News

RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.

 

Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo ya jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.

JK2

 

Maraisi wengine waliowahi kupata hiyo kutoka Chuo hicho ni Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati  Nelson Mandela.

Comments are closed.