JK AWAAPISHA WENGINE IKULU LEO

JK AWAAPISHA WENGINE IKULU LEO

Like
324
0
Wednesday, 16 September 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha bwana Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, na Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Kabla ya uteuzi huu, bwana Kyuki alikuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria na Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya uandishi wa Sheria.

Uteuzi huo umefanyika jana na umeanza mara moja.

Comments are closed.