JK AZINDUA RASMI SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 2014

JK AZINDUA RASMI SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 2014

Like
410
0
Friday, 13 February 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta, Jakaya Mrisho Kikwete, amezindua rasmi sera ya elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 2014 uliokwenda sambamba uzinduzi wa maabara 3 za Sayansi katika shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Kikwete amesema Elimu bora ni nyenzo muhimu katika maisha ya kila siku pamoja na kuliletea Taifa maendeleo kwakuwa inamgusa kila mtu bila kujali jinsia.

Uzinduzi huo uliofanywa na Rais Kikwete, ni moja ya mikakati ya kufikia malengo ya Utoaji wa Elimu bora.

Comments are closed.