JK KULIHUTUBIA TAIFA JUMATATU DECEMBER 22

JK KULIHUTUBIA TAIFA JUMATATU DECEMBER 22

Like
246
0
Friday, 19 December 2014
Local News

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, mwaka huu.

Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa rais Kikwete angefanya mazungumzo hayo leo huku baadhi ya wadau na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wakitabiri kuwa huenda hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.

Comments are closed.