JK KUMLINDA MUHONGO???

JK KUMLINDA MUHONGO???

Like
931
0
Tuesday, 23 December 2014
Local News

RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kumuwajibisha kwa kumfukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kutokana na uzembe kazini na kusababisha upotevu wa mabilioni ya fedha kama alivyofanya kwa Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi profesa Anna Tibaijuka.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Alliance For Democratic Change- ADC Said Miraji alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mtazamo wa chama hicho juu ya hotuba ya Rais kwa wananchi kupitia wazee.

Amesema kuwa chama kimeshangazwa na kitendo cha Rais kumuwajibisha waziri Tibaijuka huku akiwaacha Waziri Muhongo na katibu mkuu wa Wizara hiyo Eliakimu Maswi.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama cha Nccr-Mageuzi David Kafulila amesema kuwa hoja ya Rais kuwa Profesa Muhongo atamtoa baada ya uchunguzi wa Ikulu kukamilika ni Mbinu za kumlinda .

Comments are closed.