JK: SERIKALI ITAHAKIKISHA INADHIBITI MTANDAO WA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

JK: SERIKALI ITAHAKIKISHA INADHIBITI MTANDAO WA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Like
244
0
Tuesday, 03 March 2015
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE amesema Serikali itahakikisha inadhibiti Mtandao wa Mauaji ya watu wenye Ulemavu wa ngozi na kuitaka jamii iungane katika vita hiyo kwa kuwa ni vitendo visivyovumilika na vinalifedhehesha Taifa.

Rais KIKWETE ameeleza hayo katika hotuba yake kwa Taifa ya Mwisho wa Mwezi ambapo amesisitiza suala la kutokomeza mauaji na ukataji wa viungo vya Albino ni jambo linalowezekana na litategemea watu kuacha imani za Kishirikina.

Aidha katika Hotuba yake pia Rais KIKWETE amezungumzia suala la Uandikishaji wapiga kura na kusema Serikali itahakikisha inaiwezesha Kirasilimali,Tume ya Taifa ya Uchaguzi,ili itimize jukumu lake la kuandikisha Wananchi wote waliofikia umri wawe wameandikishwa katika daftari hilo,kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ya utambuzi wa Alama za Vidole-BVR.

Comments are closed.