RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mabalozi wa Afrika katika Umoja wa Mataifa kulitetea Bara hilo kwa sababu hamna mtu mwingine atakayetetea maslahi ya Afrika.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa kila nchi kuamua aina ya mfumo wa kisiasa ambao unaifaa nchi husika bila kulazimika kuwepo ukomo wa kiongozi kukaa madarakani.
Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo jana wakati alipozungumza na Mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa na mashirika yake mjini Gevena, Uswisi.