JOBU NDUGAI ATANGAZWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11

JOBU NDUGAI ATANGAZWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11

Like
287
0
Tuesday, 17 November 2015
Local News

ALIYEKUWA Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jobu Ndugai amefanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kushinda katika Uchaguzi uliofanyika leo Bungeni mjini Dodoma.

 

Mwenyekiti wa Muda wa kikao cha kumpata Spika, mheshimiwa Andrew Chenge amesema Mheshimiwa Ndugai ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 254 sawa na Asilimia 70 kati ya kura 365 zilizopigwa na wabunge wote wa Bunge hilo.

Kwa upande wake Spika wa bunge hilo Mheshimiwa Jobu Ndugai amewashukuru wabunge kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwaongoza na kwamba atahakikisha anaongoza kwa kufuata misingi na maadili ya Bunge.

Comments are closed.