JOHANNESBURG YAONGOZA KUWA NA IDADI KUBWA YA MATAJIRI AFRIKA

JOHANNESBURG YAONGOZA KUWA NA IDADI KUBWA YA MATAJIRI AFRIKA

Like
242
0
Thursday, 03 September 2015
Global News

RIPOTI iliyotolewa na benki ya AfrAsia na jarida la New World Wealth inaonesha kwamba mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ndio mji ulio na idadi kubwa zaidi ya watu matajiri barani Afrika.

Taarifa ya benki hiyo pia imebaini kuwa chanzo kikuu cha mapato makubwa kwa wananchi wa nchi hiyo ni uwepo wa dhahabu ya kutosha hali inayoifanya nchi hiyo kutimiza watu matajiri Elfu ishirini na tatu.

Aidha ripoti hiyo imeonesha nchi ya pili kuwa na watu matajiri Afrika kuwa ni Misri ikiwa na jumla ya matajiri Elfu kumi na mia mbili na nchi ya tatu ni Nigeria yenye matajiri Elfu tisa na miamoja.

Comments are closed.