JOHN KERRY AELEZEA MCHAKATO WA UCHAGUZI ISRAEL

JOHN KERRY AELEZEA MCHAKATO WA UCHAGUZI ISRAEL

Like
313
0
Wednesday, 17 December 2014
Global News

WAZIRI WA MAMBO ya Nje wa Marekani, JOHN KERRY, ameelezea upinzani wa nchi yake dhidi ya juhudi zozote alizodai zinahujumu mchakato wa uchaguzi wa Israel, huku akisema Marekani inatarajia kutakuwa na njia ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati na kuondoa wasiwasi wa Wapalestina.

Mkutano wa KERRY umewajumuisha Mkuu wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina, SAEEB ERAKAT, na mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, NABIL El-ARABI.

Kabla ya hapo, KERRY amekutana na Waziri Mkuu wa Israel, BENJAMIN NETANYAHU, mjini Rome, ambaye ameelezea upinzani mkali dhidi ya pendekezo la Palestina na Israel kutaka Umoja wa Mataifa uipe Israel muda na ratiba ya kupatikana kwa suluhisho la mataifa mawili, ikiwemo Israel kuondoa wanajeshi wake kwenye ardhi inayoikalia kwa nguvu.

Comments are closed.