JOHN KERRY AFANYA MAZUNGUZUMZO NA MFALME WA SAUDI ARABIA

JOHN KERRY AFANYA MAZUNGUZUMZO NA MFALME WA SAUDI ARABIA

Like
323
0
Monday, 16 May 2016
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amefanya mazungumzo na Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhusu mizozo ya Syria, Libya na Yemen, kabla ya mikutano ya kimataifa inayopangwa kuandaliwa wiki ijayo barani Ulaya kuhusu mizozo hiyo.

Ziara ya Kerry, ambaye pia amefanya mazungumzo na mwanamrithi wa ufalme na naibu mwanamrithi wa ufalme na waziri wa mambo ya nje, inakuja katika wakati muhimu wa kuimarisha juhudi za kudhibiti mapigano na kuhimiza mazungumzo ya kisiasa katika nchi zote tatu ambazo zimekumbwa na machafuko kwa miaka mingi.

Kerry anajaribu kuunga mkono mpango tete wa kusitishwa kwa mapigano nchini Syria ambao umekiukwa mara kadhaa na pande zote za mgogoro.

Comments are closed.