JOPO LA MADAKTARI KUTOKA MAREKANI LAANZA KUTOA HUDUMA ZA KIAFYA MWANANYAMALA

JOPO LA MADAKTARI KUTOKA MAREKANI LAANZA KUTOA HUDUMA ZA KIAFYA MWANANYAMALA

Like
219
0
Thursday, 23 July 2015
Local News

JOPO la Madaktari kutoka Hospitali mbalimbali za Marekani wameanza kutoa huduma za kiafya katika Hospitali ya Serikali ya Mwananyamala kwa Wagonjwa mbalimbali wenye matatizo ya kansa, kinywa, macho, kisukari pamoja huduma nyingine za kiafya

Wataalam hao walioshirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani na Taasisi ya Wanaawake wa Afrika ya Kupambana na Kansa-AWCA wanatarajia kuhudumia wagonjwa zaidi ya 600 katika maeneo ya Dar es salaam na Zanzibar ambapo Jopo hilo limechangia dawa zenye thamani ya takribani Milioni 200 kwa Watanzania.

Akizungumza na efm, Rais wa Jumuiya ya Wamarekani waishio Tanzania Idd Sandali amesema lengo la kuja kwa wataalam hao ni kutokana na kuona jinsi gani Watanzania wanakosa huduma hiyo kwa ukaribu na ubora.

Comments are closed.